STEPH CURRY KUKAA NJE KWA MIEZI MITATU BAADA YA KUFANYIWA UPASUAJI
Nyota wa Golden State Warriors Steph Curry amefanyiwa upasuaji wa mkono wake wa kushoto uliovunjika juzi katika mechi dhidi ya Phoenix Suns na sasa anataraji kukaa nje kwa muda wa takribani miezi mitatu.
Golden State Warriors kupitia ukurasa wao wa Twitter wameweka taarifa rasmi juu ya mchezaji huyo wakisema kuwa upasuaji wake ambao ulifanyika mjini Los Angels na Dokta Steven Shin, ulimalizika salama na ndani ya miezi mitatu atafanyiwa tathimini.

Hili ni pigo kubwa kwa timu hiyo ambayo imeanza msimu kwa kusuasua wakiwa tayari na pengo la mchezaji wao mwingine Klay Thompson ambaye aliumia katika fainali za NBA msimu uliopita dhidi ya Toronto Raptors.
Mpaka sasa Warriors wamecheza michezo mitano msimu huu na wamefanikiwa kushinda mmoja tu na kupoteza mingine minne.