WACHEZAJI WA BARCELONA WALIKUWA TAYARI KUCHELEWESHEWA MALIPO ILI NEYMAR ASAINIWE
Beki wa Barcelona Gerrad Pique amesema kuwa wachezaji walikuwa tayari kucheleweshewa malipo kama hili lingesaidia kumrudisha mchezaji Neymar klabuni hapo katika majira ya kiangazi yaliyopita.
Neymar aliondoka klabuni hapo mwaka 2017 kwa dau la rekodi la Euro 222 millioni. Barcelona walifanya kila jambo kuweza kumrudisha mchezaji huyo klabuni hapo bila mafanikio.

Pique akiongea na kituo cha radio cha Cadena Ser alisema “ Tulikuwa tupo tayari kurekebisha mikataba yetu” .
“Tusingechangia pesa ila tulikuwa tufanye mambo yawe marahisi kwa kuruhusu malipo mengine kufanyika mwaka wa pili ama watatu badala ya mwaka wa kwanza.” Hii yote ilikuwa ni ili kuisaidia klabu kutovunja sheria ya ‘Financial Fair Play’.

Barcelona ilitumia zaidi ya Pauni 200 millioni majira ya joto ikiwa ni pamoja na kuwasainisha wachezaji Frenkie de Jong toka Ajax and Antoine Griezmann toka Atletico Madrid.
‘Financial Fair Play’ inazuia vilabu kufanya matumizi kuzidi mapato wanayoingiza jambo ambalo liliibana Barcelona kuweza kumrudisha Neymar.