TYSON FURY AMPIGA BRAUN STROWMAN MECHI YAKE YA KWANZA WWE
Aliyekuwa bingwa wa uzito wa juu katika ngumi Tyson Furry ameshinda mechi yake ya kwanza katika WWE aliyopigana dhidi ya Braun Strowman katika tamasha la WWE Ceown Jewel nchini Saudi Arabia.

Katika mechi hiyo iliyojaa tambo, kejeli, ubabe na ngumi, Furry aliingia na vazi lake la kanzu uwanjani akiwa katika muonekano wa kiarabu kwa kuvalia hadi kilemba.

Ilimhitaji Tyson Furry kuweka juhudi za ziada kumkabili mbabe huyu wa WWE maarufu kama ‘monster among men’ baada ya kuonekana kuzidiwa kabla ya kuongeza juhudi ikiwa ni pamoja na kutumia mtindo wa gwiji Undertaker na kufanikiwa kushinda pambano.

Furry anatarajiwa kupambana na Deontay Wilder katika pambano lao la marudiano mwezi Februari mwakani .