SPRINGBOKS WATINGA FAINALI YA RUGBY KOMBE LA DUNIA
Kwenye Kombe la Dunia la Rugby linaloendelea nchini Japan.
Timu ya Rugby ya Afrika Kusini maarufu kama Springboks imeingia fainali kwa kuifunga Wales 16 – 19 katika mchezo wa nusu fainali.

Springboks watakutana na England katika fainali itakayochezwa Jumamosi huku Wales wakikwaana na New Zealand kuwania nafasi ya tatu siku ya Ijumaa.
