Arsenal wamepata pigo usiku wa Europa League
Timu ya Arsenal ya Uingereza imepata pigo wakati wa mchezo wa Europa League kati ya Arsenal dhidi ya Sporting CP ya Ureno, Arsenal wakiwa katika uwanja wa Emirates London jijini Uingereza wakicheza mchezo wao wa nne wa Europa League hatua ya Makundi, mshambuliaji wao Danny Welbeck aliumia vibaya.
Welbeck katika mchezo huo alicheza kwa dakika 27 tu za mwanzo na nafasi yake kurithiwa na Aubameyang aliyechukua nafasi yake, kabla ya kuumia na kushindwa kuendelea na mchezo huo, kuumia kwa Welbeck kuna tajwa kama pigo kubwa kwa Arsenal kutokana na mchezaji huyo anaweza kukaa nje ya uwanja kwa muda mrefu kiasi baada ya kuumia.
Pamoja na hilo mchezo huo ambao ulimalizika kwa matokeo ya 0-0, Arsenal walipata pigo tena baada ya Stephen Lichtsteiner kuumia dakika ya 71, bado haijajulikana Danny Welbeck ameumia kwa kiwango gani zaidi ya kusubiri vipimo zaidi vya madaktari baada ya kufanya uchunguzi.
Arsenal waliopo Group E na timu za Sporting CP, Qarabag na Vorskla Poltava, pamoja na kutoka sare ya 0-0, wanaongoza Kundi hilo kwa alama 10 wakifuatiwa na Sporting CP wenye alama 7, Vorskla alama 3 sawa na Qarabag.