DERECK CHISORA ‘WAR CHISORA’ APIGA MTU KWA KO ROUNDI YA 4
Bondia aliyekuwa akiwania ubingwa wa Dunia, Dereck Chisora, 35, maarufu kama ‘War Chisora’ amempiga aliyekuwa mshindi wa medali ya fedha katika Olympic bondia David Prince, 32, kwenye pambano la utangulizi katika ukumbi wa O2 Arena.

Ni katika raundi ya tatu Chisora alionesha kumzidi nguvu mpinzani wake na katika raundi ya nne alifanikiwa kumuangusha. Prince alifanikiwa kuinuka baada ya kuhesabiwa na refa ila upande wake ulirusha taulo ulingoni kuashiria kukubali kushindwa.

David Prince alikuwa ameshinda mapambano yake yote matatu yaliyopita kabla ya hili.
Chisora sasa anapanga kupigana na bondia Oleksandr Usy wa Ukraine ambaye amehamia katika uzani wa juu mwaka huu akitokea cruiserweight alipopigana mapambano yake yote bila kupoteza.
Tayari ameshinda pambano lake la kwanza katika uzani huu wa juu dhidi ya Chazz Witherspoon mapema mwezi huu.

Meneja wa Chisora, David Haye ambaye alikuwa bingwa wa Dunia akiongea na SkySports juu ya nani Chisora atapambana nae alisema “Natamani ngumi dhidi ya Oleksandr Usy. Litakuwa pambano zuri.

Akipigana na Oleksandr Usy atakuwa katika nafasi ya kushindania mkanda wa uzani wa juu, na hichi ndicho anachotaka.”