JOSH TAYLOR AMPIGA REGIS PROGRAIS NA KUFANIKIWA CHUKUA MIKANDA YA IBF NA WBA
Bondia wa Scotland Josh Taylor amefanikiwa kumpiga Regis kwa pointi na kufanikiwa chukua mikanda ya IBF na WBA katika uzani wa Super Lightweight pamoja na kuchukua ubingwa wa World Super Series.

Taylor alishinda kwa points 114-114, 115-113, 117-112 toka kwa majaji. Hii inamuacha Mscotland huyu akiwa hajapigwa katika mapambano yake 16 huku likiwa ndio pambano la kwanza kwa Mmarekani Regis kupoteza katika mapambano yake 25.

Upinzani ulikuwa mkali kwani licha ya kushinda Taylor amepata jeraha la jicho ambalo amepigana akiwa nalo raundi tatu za mwisho.