HAMILTON KUIBUKA BINGWA WA DUNIA LEO?
Ni katika Mexican Grand Prix ambapo dereva huyu sasa ataanza katika nafasi ya tatu nyuma ya madereva wa Ferrari na mbele ya Max Vertappen wa RedBull aliyepigwa penati ya nafasi tatu na kushuswa mpaka nafasi ya 4 akitokea nafasi ya kwanza.
Hamilton mwenye points 338, akifuatiwa na Valtteri Bottas mwenye points 274, anahitaji kumaliza ba points 14 mbele ya Bottass ili kutangazwa Bingwa wa Dunia msimu huu zikiwa bado mbio tatu zingine, USA ,Brazil na Abu Dhabi.
Huu utakuwa ni ubingwa wake wa 6 rekodi sawa na gwiji Michae Schumacher.

Ili kuweza shinda ubingwa huo leo Hamilton anahitaji nafasi hizi ili kumaliza points 14 mbele ya Bottas;
- Kushinda mbio pamoja na kumaliza kwa kasi zaidi mzunguko “fastest lap” na Bottas amalize chini ya nafasi ya tatu.
- Kushinda mbio na Bottas amalize chini ya nafasi ya nne.
- Kumaliza katika nafasi ya pili na kumaliza kwa kasi zaidi mzunguko “fastest lap” na Bottas amalize chini ya nafasi ya saba.
- Kumaliza katika nafasi ya pili na Bottas amalize chini ya nafasi ya saba.
- Kumaliza katika nafasi ya pili na Bottas amalize chini ya nafasi ya nane kama Bottas akafanikiwa kumaliza mzunguko kwa kasi zaidi ‘fastest lap’.
- Kumaliza katika nafasi ya tatu pamoja na kumaliza mzunguko kwa kasi zaidi ‘fastest lap’ na Bottas amalize chini ya nafasi ya nane.
- Kumaliza katika nafasi ya tatu na Bottas amalize chini ya nafasi ya tisa.