RIVALDO ANAAMINI KUAHIRISHWA KWA EL CLASICO KUNAINUFAISHA REAL MADRID
Mshambuliaji wa zamani wa timu ya taifa ya Brazil na Barcelona Rivaldo amenukuliwa na vyombo vya habari akizungumzia kuhusiana na kuahirishwa kwa mchezo wa El Clasico uliyokuwa uchezwe Oktoba 26 2019.
Rivaldo anaamini kupelekwa mbele kwa mchezo huo hadi Desemba 18 kutaisaidia Real Madrid zaidi kwani kama ingechezwa Oktoba 26 ingekuwa mbaya kwao kwa sababu wametoka kupoteza dhidi ya Mallorca hivyo wasingekuwa katika ubora na kujiamini sana ila kusogezwa mbele kunawafanya wajipange zaidi.

“Mabadiliko (Elclasico) ni mbaya kwa Barcelona licha ya kuwa hawapo katika ubora wao ila walikuwa katika kiwango, tofauti na Real Madrid ambao wametoka kupoteza dhidi ya Mallorca, nafikiri kama ungechezwa Jumamosi hii (Oktoba) ingekuwa ni nafasi nzuri kwa Barcelona kuifunga Madrid na kuongeza tofauti ya point dhidi yao, Real Madrid wamepata bahati kidogo” alisema Rivaldo
Hadi sasa Barcelona wameshinda michezo minne mfululizo ya LaLiga hivi karibuni, ukiacha Real Madrid ambao wametoka kupoteza dhidi ya Mallorca na sare ya 0-0 dhidi ya Atletico Madrid.