HATIMAE MARTIAL KAIONDOA MANCHESTER UNITED KWENYE UKAME WA MIEZI 7
Hatimaye goli la penati la dakika ya 43 la Anthony Martial akiifungia Manchester United katika ushindi wa 1-0 dhidi ya Partizan Belgrade linarejesha tabasamu kwa mashabiki wa Man United kuona timu yao imeanza kupata matokeo ugenini.
Mashabiki wa Man United usiku huo wameshuhudia timu yao ikipata ushindi wa 1-0 ukiwa ndio ushindi wao wa kwanza ugenini baada ya miezi karibia nane.

Mara ya mwisho Man United wanapata ushindi wa ugenini ilikuwa Machi 2019 katika mechi dhidi ya PSG, toka siku hiyo walikuwa wanapoteza na kutoka sare ugenini.
Ushindi huo umeifanya pia Man United kuwa kinara wa Kundi A kwa kuwa na alama 7, huku Partizan wakiwa nafasi ya 3 kwa kuwa na alama 4, AZ Akmar akiwa nafasi ya 2 kwa alama 5 huku Astana akishika mkia kwa kuwa na alama 0.