MO DEWJI KAUKUMBUKA MCHANGO WA MAGORI SIMBA SC
Bilionea na Mwekezaji wa Simba SC MO Dewji ameonekana kuukumbuka mchango wa Crescentius Magori licha ya kumaliza muda wake kama CEO wa Simba SC na kukaa pembeni.
Oktoba 24 2019 Mo Dewji kupitia ukurasa wake rasmi wa instagram amemtangaza rasmi Magori kuwa ndiye mshauri wake katika mambo yake ya soka wakati huu MO Dewji akiwa mwenyekiti wa bodi ya Simba SC.
Napenda kutangaza rasmi kuwa nimemteua Crescentius Magori kuwa mshauri wangu binafsi kama Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Simba. Anauzoefu mkubwa wa soka na uwepo wake utaongeza nguvu kwenye safari yetu ya kuifanya Simba kuwa moja ya klabu yenye mafanikio makubwa Afrika. pic.twitter.com/54wc2SNqqQ
— Mohammed Dewji MO (@moodewji) October 24, 2019
“Napenda kutangaza rasmi kuwa nimemteua Ndg. Crescentius Magori kuwa mshauri wangu binafsi kama Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Simba. Ana Uzoefu mkubwa wa soka la Afrika na ninaamini uwepo wake utaongeza nguvu kwenye safari yetu ya kuifanya Simba kuwa moja ya klabu yenye mafanikio makubwa zaidi barani Afrika” aliandika MO Dewji