LALIGA HAWAJAPENDEZWA NA UAMUZI WA RFEF KUHUSU EL CLASICO
Shirikisho la mchezo wa mpira miguu nchini Hispania (RFEF) baada ya kukaa limepitisha tarehe mpya ya mchezo wa El Clasico wa FC Barcelona dhidi ya Real Madrid uliyokuwa awali uchezwe Oktoba 26 Nou Camp lakini ukaahirishwa kutokana na machafuko ya kisiasa Catalunya.
RFEF kwa kushirikiana na kamati ya mashindano wametangaza sasa mchezo wa kwanza wa msimu wa El Clasico 2019/2020 utachezwa Desemba 18 katika uwanja huo huo wa Nou Camp.
Baada ya maamuzi hayo ,LaLiga wameonekana kutokubaliana na hilo na wanajipanga kuchukua hatua za kisheria.

LaLiga walipendekeza mechi hiyo ichezwe Disemba 4, kwani Tarehe 18 Disemba raundi ya kwanza ya Copa del Rey inataraji kuanza.
LaLiga wameeleza kuwa hawajakubali kwa moyo mmoja kupangwa mchezo huo kuchezwa Desemba 18 na wanaweza kuchukua hatua zaidi za kisheria ikiwemo kukata rufaa kama watajiridhisha na kuona haja ya kufanya hivyo kwani hawajahusika na hilo zaidi ya kamati ya mashindano kujadiliana tu na Barcelona na Madrid basi.