Tamaa imewaponza Everton yafungiwa miaka miwili.
Klabu ya Everton inayoshiriki Ligi Kuu Uingereza imefungiwa kusajili kwa miaka miwili baada ya kugundulika imevunja sheria za Ligi Kuu Uingereza, hii ni baada ya uchunguzi kufanyika na kugundulika wamefanya ujanja ujanja.
Everton wamefungiwa kwa kipindi cha miaka miwili kusajili wachezaji wa Academy wenye umri kati ya miaka 10-18, baada ya kugundulika kuwa staff wa Academy yao walikuwa wametoa ofa kwa mchezaji (mtoto) na familia yake na kuanza kumshawishi ili ajisajili na timu yao ya kinyume na taratibu.
Timu hiyo haitaruhusiwa katika kipindi cha miaka miwili kumsajili mchezaji yoyote wa Academy au Academy yoyote ya soka iliyomsajili kwa zaidi ya miezi 18, hata hivyo adhabu hiyo imeenda sambamba na faini ya pound 500,000, Everton sasa wanaungana na timu za Liverpool na Manchester City ambazo nazo zimekumbana na adhabu kama hiyo.
Everton tayari wameomba msamaha na kukiri kosa lakini mkuu wa usimamizi wa Academy yao Martin Waldron anaendelea kusimamishwa kutokana na kuhusika na kosa hilo (Tapping-up), kijana aliyeshawishiwa ajiunge na Everton kwa sasa anacheza Manchester United.
Tapping Up ni kitendo cha kumshawishi mchezaji wa timu Fulani kujiunga na timu yako pasipo klabu yake husika kujua, hilo ndio kosa walilolitenda Everton klabu ambayo imemlea na kuibua kipaji cha nahodha wa zamani wa Uingereza Wayne Rooney.