KMC wamemwaga mboga Humud kamwaga Ugali
Kiungo wa zamani wa KMC ya Kinondoni Abdulhalim Humud amejibu tuhuma zinazomkabili mbele ya waandishi wa habari kuhusiana na tuhuma kutoka katika timu yake hiyo ya KMC ambayo amevunja nao mkataba hivi karibuni kwa shutuma za utovi wa nidhamu.
Abdulhalim Humud alituhumiwa pia kudaiwa kuiba namba ya simu ya mpenzi wa mchezaji mwenzake kutoka katika simu ya mchezaji mwenzake, kisha kuanza kumsumbua, kitu ambacho kilipelekea pia KMC kuridhia ombi lake la kuvunjwa kwa mkataba.
Leo Humud amejibu tuhuma hizo na kuzikanusha kwa kusema kuwa kuna matatizo ndani ya KMC hivyo anadaiwa wamedharia kumchafua, Humud amefika mbali zaidi na kueleza kuwa hajawahi kufanya hivyo au kuwatakana mashemeji zake au wapenzi wa marafiki zake.
Humud katika mkutano na waandishi wa habari aliambatana na meneja wake kutoka Mtembezi Sports Management Mr Antonio Nugaz “Mimi nilitoka nikaenda kwa meneja wangu tukajadili na nikaenda kuwaomba waniruhusu kwenda kutafuta maisha sehemuy nyingine hilo lilikuwa ombi”alisema Humud
“Kingine ni shutuma za kusema mimi nachukua wake za watu kitu ambacho kimenichafulia mimi familia yangu na marafiki zangu kwa ujumla , hiyo hiko ni kitu sio cha kweli mimi ni muungwana siwezi kufanya kitu kama hicho nadhani kama kiongozi wa mpira sio kitu sahihi maana mambo ya mpira yanatakiwa yamalizike kwenye mpira huwezi kuleta mambo ya mapenzi katika mpira”alisema Humud
“Niseme tu hili halipo sawa na sio sahihi kikubwa ni kwamba wakati naenda pale na uongozi ulikuwa umebadilika nilikutana masuala ya rushwa, mimi sio mchezaji ambaye naweza kutoa rushwa hili mimi nicheze nigawane na wewe signing fee kusudi tu nicheze na niwe rafiki yako”alisema Humud
Tukukumbushe kuwa Abdulhalim Humud alianza kufahamika zaidi miaka 10 iliyopita baada ya ujio wa kocha mbrazil Marcio Maximo katika timu ya Taifa ya Taifa Stars na kuanza kumuamini na kumuita kikosini, Humud amewahi kucheza soka katika timu mbalimbali Tanzania kama Ashanti United, Mtibwa Sugar, Simba SC na Azam FC.