Chirwa atambulishwa rasmi Azam FC
Mshambuliaji wa zamani wa Yanga SC Obrey Chirwa amejiunnga na Azam FC kwa mkataba wa mwaka mmoja.
Raia huyo wa Zambia ametambulishwa leo mbele ya waandishi wa habari jijini Dar es salaam.
Chirwa anajiunga na Azam FC huku akiziacha fununu zilizokuwa zimeenea kuwa angeweza kurejea kwenye klabu yake ya zamani Yanga hata kama Kocha wao Mwinyi Zahera alishaweka msimamo wake wazi kuwa asingefurahishwa kama mchezaji huyo angerejea klabuni hapo