GERARD PIQUE ATAFUTA KADI ILI ASISOKE EL CLASICO
Barcelona wamebakisha kucheza mechi moja tu katika LaLiga kabla ya kucheza El Clasico ya kwanza msimu huu.
Katika kuhakikisha anacheza mechi hiyo ya El Clasico, beki wa Barcelona Gerard Pique jana aliitafuta kadi ya njano katika mchezo dhidi ya Sevilla, na kuipata baada kuupiga mbali mpira uliokuwa umetoka katika dakika za mwisho.
Pique aliitafuta kadi hiyo ya njano ambayo ni ya tano kwake katika msimu huu, na hivyo itamfanya atumikie adhabu ya kukosa mechi moja inayofuata ambayo watacheza dhidi ya Eibar Oktoba 19.
Kwa kufanya hivyo sasa ana uhakika wa kucheza mechi ya El Clasico itakayochezwa Camp Nou Oktoba 26.