WACHEZAJI WATANO WA ERITRIA WAZAMIA UGANDA
Wachezaji watano wa timu ya taifa ya Eritrea U-20 wamepotelea Jinja nchini Uganda siku moja kabla ya kumalizika kwa CECAFA U-20 Tanzania ikiwa Bingwa.
Hadi Eritrea anacheza mechi dhidi ya Sudan ya kutafuta mshindi wa tatu hapo alikuwa na wachezaji 15 kati ya 20, watano kati yao wakidaiwa kutorokea nchini Uganda kwa ajili ya kutafuta maisha.
Tukio hilo lilifanya CECAFA kuwaongezea ulinzi zaidi wachezaji wa Eritrea ili wasije kutoroka.
Hii sio mara ya kwanza katika historia ya michuano ya CECAFA wachezaji kutoka Eritrea kudaiwa kutoroka.