Hazard kaungana na timu kuelekea beralus
Kiungo wa mshambuliaji wa Chelsea Eden Hazard imethibitika kuwa atakuwa sehemu ya kikosi cha Chelsea kitakachocheza mchezo wa Europa League nchini Beralus dhidi ya BATE Borisov.
Vijana hao wa Maurizio Sarri ambao wanaongoza katika Group lao baada ya kucheza michezo mitatu ya mwanzo, wamejumuika na Eden Hazard katika safari ya Belarus baada ya mchezaji huyo kuhofiwa kuwa na majeruhi ya mgongo yaliokuwa yanamsumbua toka mwezi uliopita baada ya mchezo dhidi ya Manchester United uliomalizika kwa sare ya 2-2.
Pamoja na kuwa Hazard alicheza mchezo wa Crystal Palace Jumapili hii kwa dakika 26 alikuwa ana hofiwa kuwa bado hayuko timamu kwa asilimia 100 hivyo ingewezekana kaachwa London kwa ajili ya kujiandaa kuimarisha utimamu wa mwili wake baada ya kupona majeraha.
Hazard Jumatano asubuhi alionekana Cobham akiingia kwenye basi la timu hiyo kwa ajili ya kuelekea uwanja wa ndege na kuanza safari ya kuelekea Minsk Belarus kwa ajili ya mchezo dhidi ya BATE Borisov, pamoja na yote hali ya hewa ya nchi ya Belarus iliyopo Mashariki mwa Ulaya inatajwa kufikia hadi sifuri temperature.
Chelsea kwa sasa wapo nafasi ya kwanza katika Group L wakiwa na jumla ya alama 9 baada ya ushindi wa michezo yao yote mitatu ya mwanzo, wakifuatiwa na PAOK, MOL Vidin na BATE Borisov.