HAT TRICK DHIDI YA YANGA YAMLIPA NCHIMBI
Zikiwa zimepita saa chache tangu kufunga Hat Trick dhidi ya Yanga, mshambuliaji wa Polisi Tanzania Ditram Nchimbi ameongezwa katika kikosi cha Taifa Stars kilichotajwa na kocha Etienne Ndayiragije jana kwa ajili ya mechi ya kirafiki dhidi ya Rwanda itakayochezwa Oktoba 14 jijini Kigali.Nchimbi jana aliweka rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza kufunga Hat Trick katika ligi kuu Tanzania bara msimu huu.