CAS IMEAGIZA KENYA KUMLIPA FIDIA KOCHA WAO ADEL AMROUCHE LA SIVYO WATATOLEWA KATIKA KUFUZU KOMBE LA DUNIA
Mahakama ya michezo duniani CAS imeliagiza shirikisho la soka nchini Kenya FKF kumlipa fidia aliyekuwa kocha wao Adel Amrouche baada ya kumfuta kazi mwaka 2014.
Amrouche alifukuzwa baada ya Kenya kutolewa na Lesotho katika safari ya kufuzu michuano ya mataifa Afrika 2015.
Kipindi anafukuzwa alikuwa ametumikia Kenya miezi 18 katika kandarasi yake ya miaka mitano aliyokuwa amesaini.
CAS imeitaka FKF kumlipa fidia ya USD Milioni 1.08 (Tsh Bilioni 2.4) Mbelgiji huyo ambaye kwa sasa ni kocha wa timu ya taifa ya Botswana.
Agizo la CAS kwenda FKF linatakiwa litekelezwe hadi mwisho wa mwezi Oktoba na endapo wasipofanya hivyo wataondolewa katika mbio za kuwania kucheza fainali za Kombe la Dunia 2022 (WCQ) zitakazofanyika Qatar.
.
“Tutawaomba FIFA watupe muda zaidi. Tunalipa (pesa) kwa makosa ya uongozi uliopita. Nitazungumza na serikali na kuwaomba watusaidie katika kumlipa Amrouch,” amesema Rais wa sasa wa FKF Nick Mwendwa.