WAMBURA KAKUBALI YAISHE KAANDIKA BARUA YA DPP
Baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania DR John Pombe Magufuli kutoa ushauri kwa Mkurugenzi wa Maashtaka nchini (DPP) kuwa kwa wale watuhumiwa wa makosa ya uhujumu uchumi watakaokuwa tayari kukiri kosa na kurejesha fedha basi wasamehewe, jana Oktoba 2 aliyekuwa makamu wa Rais wa TFF Michael Richard Wambura ameiambia Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu chini ya hakimu mfawidhi Kelvin Mhina kuwa ameandika barua ya kukiri kosa kwa DPP na kuomba msamaha.
Baada ya kueleza hivyo , kesi yake imeahirishwa hadi Oktoba 16 2019.
Wambura alifikishwa Mahakamani Februari 11 2019 kwa tuhuma ya makosa 17 likiwemo la utakatishaji fedha zaidi ya Tsh Milioni 100 wakati akiwa kiongozi wa soka.