FRANK LAMPARD KAWEKA REKODI CHAMPIONS LEAGUE
Timu ya Chelsea usiku wa Oktoba 2 2019 walikuwa Ufaransa kucheza mchezo wao Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Lille uliyomalizika kwa Chelsea kupata ushindi wa magoli 2-1.
Magoli ya Chelsea yakifungwa na Abraham na Willian na kufanya Chelsea ikiondika na alama 3 na huo kuwa ushindi wao wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa msimu huu.
Ushindi huo Chelsea iliyochini ya kocha wake Frank Lampard inaweka rekodi ya kuwa kocha wa kwanza wa England kupata ushindi Ligi ya Mabingwa Ulaya toka Machi 2017 Craig Shakespeares afanye hivyo akiwa na Leicester City kwa kuifunga Sevilla.