KCM KUJENGA UWANJA WAO UTAKAOKAMILIKA 2020
Klabu ya soka ya KMC inayomilikiwa na Manispaa ya Kinondoni baada ya kuwa na msimu mzuri wa Ligi 2018/2019 na kumaliza nafasi ya 4 wakishiriki mara ya kwanza, sasa wameonesha dhamira yao ya kutaka kufikia malengo ya juu zaidi.
KMC sasa imeonesha ramani ya Ujenzi wa uwanja wao utakaojengwa eneo la Mwenge jijini Dara es Salaam.
Ujenzi wa uwanja huo unatazamiwa kukamilika mwaka 2020 ukiwa na uwezo wa kuchukua mashabiki 3000 na thamani yake unatajwa kuwa unakadiriwa kufikia Tsh Bilioni 3.