WILDER KUTETEA UBINGWA WAKE DHIDI YA LUIS ORTIZ NOVEMBA 23
Bondia Mmarekani Deontay Wilder, 33, anayeshikilia ubingwa wa WBC tokea mwaka 2015, atapigana na Mcuba Luis Ortiz Novemba 23 mwaka huu Las Vegas kutetea taji hilo.
Wilder ana rekodi ya kushinda mapambano 41, kutoa sare 1 akiwa hajapoteza lolote na pambano la mwisho baina yake na Ortiz liliisha kwa Wilder kushinda kwa Knock Out jijini NewYork.

Wilder amepigana mapambano mawili tokea kipindi hicho moja likiwa dhidi ya Muingereza Tyson Furry Disemba 2018 pambano lililoisha kwa sare na lingine likiwa dhidi ya Dominic Breazeale Mei 2019 ambapo alishinda kwa KO.
“Anatakiwa kuwa kamili kwa raundi 12. Mimi ninatakiwa tu kuwa kamilifu kwa raundi mbili. Nimezawadiwa na zawadi ya nguvu,” alisema Wilder alipokuwa akiongelea pambano lake na Ortiz.