Mourinho akiri alitukanwa wakati wa mchezo wa Manchester United dhidi ya Juventus.
Kocha wa Manchester United baada ya mchezo wao na uventus kumalizika kwa wao kupata alama tatu kufuatia ushindi wa magoli 2-1, magoli yao yakipatikana ndani ya dakika nne za mwisho kabla ya mchezo kumalizika, wengi walitaka kufahamu kwa nini alianza kejeli zake.
Jose Mourinho ni aina ya walimu wa soka wenye kejeli sana pale anapokuwa amefanikiwa kumfunga mpinzani wake, hivyo baada ya dakika 90 kuisha na Manchester united kuondoka na alama tatu, mourinho alianza kuwakosoa mashabiki wa juventus kwa kuweka mkono wake wa kulia katika sikio lake la kulia ikitafsiriwa kuwa ni kejeli ya kuwataka waendelee kushangilia na kumkosoa tena kama walivyokuwa wanafanya.
Mchezo ulivyomalizika na mourinho alipotoka uwanjani alilazimika kujibu kwa nini alifanya vile baada ya ushindi, Mourinho alieleza kuwa alifanya vile kutokana na matusi aliyokuwa anayapata wakati wa mchezo na kusema kuwa yaligusa hadi familia yake na Inter milan ambayo aliwahi kuifundisha mwaka 2008-2010.
“Nilitukanwa kwa dakika 90 nilikuja hapa kufanya kazi yangu na sio kingine cha zaidi, nilifanya lugha ya ishara kuonesha nataka kuwasikia wao kwa sauti ya juu zaidi, kama wasingenitusi yamkini nisingeweza kufanya vile, kwa kichwa kilichotulia nisingeweza kufanya vile lakini familia yangu ilitukanwa pamoja na familia yangu ya Inter ndio maana nikakasirika na kufanya kama vile”alisema Mourinho