UGANDA HATIMAE YAPATA KOCHA MPYA
Shirikisho la mpira wa miguu nchini Uganda (FUFA) leo limetangaza kumpata kocha mpya Jonathan Mckinnstry baada ya kuchukua nafasi ya Sebastian Desabre.
Uganda waliachana na Sebastian Desabre baada ya timu ya taifa ya Uganda The Cranes kutolewa raundi ya 16 Bora katika michuano ya AFCON 2019 iliyofanyika nchini Misri.
Jonathan Mckinnstry,34,ambaye ni raia wa Ireland Kaskazini,amewahi kuzifundisha timu za Taifa za Sierra Leone (2013-14) na Rwanda (2015-16).