OLE GUNNAR SOLSKJAER MAMBO YANAZIDI KWENDA KOMBO
Kocha wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer kwa sasa yupo katika wakati mgumu kufuatia kusuasua kwa timu yake toka alipokabidhiwa jumla kama kocha mkuu baada ya kukaimu kwa miezi kadhaa.
Solskjaer ana wakati mgumu baada ya sare ya 1-1 dhidi ya Arsenal waliosawazisha goli dakika ya 58 kupitia kwa Pierre Aubameyang katika uwanja wa Old Trafford wakati Manchester United walikuwa wanaongoza kwa goli lililopatikana dakika ya 45 kupitia kwa McTominay.
Sare hiyo inaiweka Manchester United katika nafasi ya 10 katika msimamo wa Ligi Kuu ya nchini England wakiwa na alama 9 wakicheza michezo 7 na kushinda miwili, sare 3 na wamepoteza michezo miwili.
Unaweza kusema Solskjaer kakalia kuti kavu kutokana na Manchester United kuwa na takwimu mbaya toka mwezi Machi 2019 akabidhiwe timu jumla kama kocha mkuu, huu ukiwa ni mchezo wake wa 15 akishinda michezo minne pekee.