REFA KAWAONESHA KADI NYEKUNDU BALL BOYS
Ni tukio ambalo halijazoeleka kuonekana likitokea michezoni lakini mwamuzi wa mchezo wa National League kati ya Yeovill Town dhidi ya Bromley juzi Jumamosi, Aaron Jackson kathubutu.
Mwamuzi Aaron Jackson amefikia maamuzi ya kuwaonesha kadi nyekundu ball boys (wavulana wanaookota mipira wakati wa mechi) wa Yeovil Town kutokana na kuhusika kuchelewesha muda katika mchezo huo ambao Yeovil Town wakiwa nyumbani,walipata ushindi goli 3-1.
https://twitter.com/YTFC/status/1177976553738817536
84 | The referee has, no joke, just sent off one of our ball boys…
(3-1) #YTFC— Yeovil Town FC (@YTFC) September 28, 2019
“Ball Boy mmoja alikuwa anachelewesha kumpa mpira mchezaji wa Bromley Sam Wood dakika 10 za mwisho na mwamuzi kumpa onyo.
Pale Ball Boy yule yule aliporudia kile kile muda mchache baadae, mwamuzi akaamua kuagiza Ball Boys (wote nane) watolewe nje ” alisema mchambuzi wa BBC Chriss Spittles.
Baada ya mwamuzi kutoa agizo hilo,mlinzi mmoja wa uwanjani akawakusanya wote na kuwatoa uwanjani.