KOCHA WA DAVID DE GEA AONDOKA MAN UNITED
Kocha wa kipa wa Manchester United David De Gea, Mhispania Emilio Alvarez ameondoka katika timu hiyo, wamethibitisha Man United.
Alvarez,47, ameripotiwa kuondoka Man United baada ya maswali kuja juu ya mbinu zake za ufundishaji kufuatia kiwango cha David De Gea kushuka kuanzia msimu uliopita.
Mhispania huyo alijiunga na Man United mwaka 2016 kuungana na De Gea ambaye amekuwa akimfundisha tangu alipokuwa anaichezea Atletico Madrid.
De Gea amewahi kumsifia Alvarez kuwa ndiye amemfanya kuwa moja ya makipa bora duniani.
Kocha mkuu wa Man United Ole Gunnar Solskjaer mwezi Juni alimrudisha klabuni kocha wa zamani wa Academy yao, Richard Hartis ili kuwa kocha wa makipa katika kikosi cha kwanza,hii ilianza kuleta vitisho katika kibarua cha Alvarez.