ERNESTO VALVERDE ASHINDWA KUJUA MESSI ANARUDI LINI
Mshindi mara tano wa tuzo ya Ballon d’Or Lionel Messi bado yupo katika wakati mgumu kufuatia kuanza msimu mpya wa 2019/2020 kwa kuwa majeruhi.
Baada ya kuumia hivi karibuni katika mchezo dhidi ya Villarreal kocha wake Ernesto Valverde ameweka wazi maendeleo ya majeraha yake.
Kocha Ernesto Valverde amesema hajui ni lini mchezaji huyo atarudi dimbani lakini amedai tatizo alilolipata si kubwa sana.
Katika mchezo huo wa ligi uliochezwa Jumanne ya wiki hii, Lionel Messi alipata maumivu katika nyama za paja, na kumfanya acheze dakika 45 tu katika mechi hiyo ambayo walishinda kwa goli 2-1.
Mpaka sasa msimu huu Lionel Messi hajacheza dakika 90 katika mechi na alikosa mechi nne za mwanzo wa msimu kwa kuumwa shavu lake la mguu.