Mashabiki waandaa kituko ili kushinda mechi.
Timu yako inapocheza na vinara wa ligi ni muhimu kuwa na mchezaji wa 12, lakini mashabiki wa timu hii walichokifanya ni kitu cha kushangaza zaidi.
Wikiendi hii, katika ligi daraja la 3 huko Uholanzi, timu ya Rijnsburgse Boys waliopo nafasi ya saba kwa ligi waliwakaribisha vinara wa ligi AFC katika uwanja wao wa nyumbani.
Mashabiki wa Rijnsburgse Boys wakaandaa kitu kisicho-kawaida ili kuwaharibu wachezaji wa timu pinzani, walimuajiri ‘stripper’ kukatiza uwanjani muda wa mechi akiwa uchi kabisa huku akiwa amebeba bendera ya timu yao.
Wakati wa mechi, AFC Amsterdam walikuwa wanajiandaa kupiga ‘free-kick’ , mashabiki wa timu hiyo ya nyumbani wakaanza kurusha karatasi nyeupe uwanjani, na hapo hapo mwanadada huyo ‘ stripper’ akaruka kuingia uwanjani na kuanza kuwasumbua wachezaji wa timu pinzani ili kuwaondolea umakini.
Mwanadada huyo akiwa uchi huku amebeba bendera ya timu hiyo ya nyumbani alikatiza na kuwasumbua wachezaji kwani walisimama na kuanza kumuangalia, wengi walimshangaa.
Baada ya mechi kuisha, mwanamke huyo aliviambia vyombo vya habari kuwa kitu alichokifanya ni kazi ambayo alilipwa.
“ Baada ya kukatiza uwanjani, nikaenda kuendelea na kazi yangu nyingine. Huwa ninafanya ‘strip shows’ . Lakini hii ilikuwa tofauti. Ningependa kuifanya tena . “ Mwanamke huyo aliwaambia waandishi.