FIFA INAFIKIRIA KUBADILI KANUNI ZA USAJILI
Shirikisho la mchezo wa miguu duniani FIFA linaripotiwa kuwa katika mpango wa kubadili kanuni za usajili wa wachezaji ikiwemo wanaokwenda kwa mkopo na pia kuhusu mawakala
Mabadiliko mapya yanalenga kwenda kupunguza kiwango cha pesa (commision) wanachopata mawakala dili la mteja wao (mchezaji) linapokamilika lakini sambamba na kuweka idadi ya wachezaji wanaopaswa kutolewa kwa mkopo kwa msimu mmoja, ada atakayostahili kupewa wakala ni asilimia 10 ya pesa za usajili zinazolipwa kwa timu inayomuuza mchezaji.
Imeelezwa kuwa kwa wachezaji wenye miaka 22 na kuendelea,
kuanzia msimu ujao klabu zitaruhusiwa wachezaji nane tu kwa mikopo ya kimataifa, ( kusajili kwa mkopo na kutoa kwa mkopo), ambapo baada ya miaka miwili watapungua mpaka sita.
Kamati ya FIFA tayari imewasilisha mapendekezo hayo kwa baraza la FIFA ambalo litakutana kujadili Oktoba 24.