Xhaka apewa kitambaa Arsenal
Kocha mkuu wa Arsenal Unai Emery amemtangaza Granit Xhaka kuwa nahodha wa kudumu wa klabu hiyo.
Unai amekitangazia kikosi cha Arsenal maamuzi hayo leo asubuhi kuelekea mechi yao ya jumatatu dhidi ya Man United Old Trafford.
Xhaka ambaye ametimiza umri wa miaka 27 leo, ameiongoza Arsenal katika mechi sita kati ya nane walizocheza msimu huu, lakini Unai alikuwa bado hajatoa maamuzi ya kumpa unahodha kwa kudumu.
Mswiss huyo anachukua kitambaa hicho ambacho kilikuwa kinavaliwa na Laurent Koscielny ambaye amejiunga na Bourdaux majira haya ya kiangazi.