MO SALAH ARUSHA KIJEMBE KWA CHAMA CHA SOKA MISRI
Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Misri na klabu ya Liverpool ya nchini England Mohamed Salah ameandika ujumbe unaonekana kuwa ni kukasirishwa na shirikisho la soka nchini kwake EFA kwa kutoona kura zao tuzo za The Best za FIFA.
Kwa kawaida tuzo ya The Best FIFA yaani ya mchezaji bora wa FIFA mshindi kupatikana kwa makocha na manahodha wa timu za taifa kupiga kura kumtafuta mshindi na muda mchache baadae FIFA huonesha kila mpiga kura alimchagua mchezaji gani.
Lionel Messi ndiye aliyeibuka mshindi wa tuzo hiyo mwaka huu, Salah akishika nafasi ya nne akipitwa pointi 20 na Lionel Messi
Kura za kocha wa Misri Shawky Gharib na nahodha wao Ahmed Elmohamady hazijaonekana katika orodha ya wapiga kura iliyotolewa na FIFA,na hivyo kupelekea Salah kukasirishwa na chama cha cha soka cha Misri EFA.
Kufuatia kitendo hicho,Salah ameondoa viashiria na vielelezo vyote vya Misri katika ‘bio’ yake ya Twitter na sasa ameandika ‘Footballer for Liverpool’.
.
Kupitia kurasa wa Twitter Mo Salah ameandika “Chochote wanachofanya kujaribu kubadili mapenzi yangu kwa Misri, hawatafanikiwa”
.
Baada ya hilo EFA ilituma maswali yao FIFA itolee ufafanuzi kukosekana kwa kura zao ambazo walizituma Agosti 15,2019.
EFA wanasema kocha na nahodha wa Misri wote walimpigia Mo Salah katika nafasi ya kwanza.
Kwa upande wa FIFA imeelezwa kuwa fomu za EFA hazikupitishwa kwa sababu sahihi zao zilikuwa kwa herufi kubwa na pia hakukuwa na sahihi ya katibu mkuu wao.
.
“Chama cha soka cha Misri kilipokea ukumbusho mara mbili wa kuwasilisha fomu zilizosainiwa vizuri kabla ya Tarehe 19,Agosti,2019.
EFA hawakuwasilisha fomu hizo kwa muda uliopangwa mpaka 21,Agosti,2019. Kwa hiyo kura kutoka EFA hazikuhesabiwa” Msemaji wa FIFA aliiambia Reuters.