KOCHA KASIMAMISHWA KAZI ENGLAND KWA KUTUHUMIWA KABET
Klabu ya AFC Wimbledon inayoshiriki League One nchini England imeamua kumsimamisha kazi kocha wake mkuu Wally Downes kwa kutuhumiwa kuwa amejihusisha na masuala ya ubashiri (betting) kinyume na taratibu za FA.
Kwa kawaida viongozi wa soka makocha na wachezaji wa soka au muajiriwa yeyote kwenye masuala ya soka ambaye anaweza kwa namna moja au nyinge akachochea upangaji wa matokeo haruhusiwi kufanya ubashiri.
Baada ya FA kumtuhumu Wally Downes kuwa alibashiri (betting) jumla ya mikeka nane tofauti kati ya kipindi cha Novemba 2014 hadi Julai 2019, Wally amepewa hadi Oktoba 4 2019 kuwasilisha utetezi wake, wakati huu klabu yake ikiwa imemmsimamisha na nafasi yake kuwa chini ya Glyn Hodges kuelekea mchezo wa Jumamosi dhidi ya Peterborough.