JURGEN KLOPP AINGIA TAASISI YA JUAN MATA KWA KISHINDO
“Ninatangaza kwamba kuanzia leo na kuendelea mimi ni memba wa familia ya Common goal” hayo ni maneno ya kocha wa Liverpool Jurgen Klopp jana mjini Milan baada ya kukabidhiwa tuzo ya FIFA ya kocha bora wa kiume wa mwaka 2019.
Common Goal ni taasisi ya misaada iliyoanzishwa na kiungo wa Man United Juan Mata Agosti 2017 ambapo wanasoka na makocha huchangia asilimia 1 ya mishahara yao kwa ajili ya kusaidia jamii zilizo katika hali mbaya duniani kote ili waweze kubadili na kuboresha maisha yao.
Baada ya kusema maneno hayo Klopp akapigiwa makofi na watu waliokuwepo ukumbini, baada ya hapo kocha huyo akasema : “ Ni watu wachache wanaijua hii (Common goal), kama haujui, Google. Ni kitu kizuri’.
.
Dakika chache baada ya kutamka maneno hayo, tovuti ya Common goal ikakwama (Crashed) kufuatia kuzidiwa uwezo kutokana na wingi wa watu waliokuwa wakiingia katika tovuti hiyo.
Baada ya muda kidogo tovuti hiyo ikarudi na kukaa vizuri.
Klopp ambaye inaelezwa kuwa anapokea mshahara wa Pauni milioni 10 kwa mwaka (Tsh Bilioni 28.6), amekuwa ni kocha wa kwanza kutoka ligi kuu nchini England kujiunga na taasisi hiyo.
Wengine kutoka ligi kuu ya England ambao wapo ni kipa Kasper Schmeichel wa Leicester City ,Charlie Daniels wa Bournemouth na Leon Balogun wa Brighton.
Majina mengine ni Mats Hummels,Megan Rapinoe,Alex Morgan,Giorgio Chiellini,Serge Gnabry,Shinji Kagawa,Rais wa UEFA Aleksander Ceferin