LIONEL MESSI KASHINDA FIFA THE BEST KWA MARA YA KWANZA KATIKA HISTORIA
Nahodha wa klabu ya FC Barcelona ya nchini Hispania na timu ya taifa ya Argentina Lionel Messi amefanikiwa kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa mwaka wa shirikisho la soka ulimwenguni FIFA (FIFA The Best) kwa mara ya kwanza toka mfumo mpya wa utolewaji wa tuzo hiyo uanze kutumika, toka pale ilipotenganishwa na Ballon d’Or 2016.
Messi ameshinda tuzo hiyo mbele ya mpinzani wake mkuu Cristiano Ronaldo ambaye hakuwepo katika utoaji wa tuzo hizo sambamba na Virgil van Dijk wa Liverpool na kutangazwa mshindi na Rais wa FIFA Gianni Infantino.
Tuzo hiyo imetolewa kwa kuangalia wachezaji waliofanya vizuri kuanzia Julai 16 2018 hadi Julai 19 2019, uwezo na jitihada binafsi zimemfanya Messi aonekane bora, msimu uliompa tuzo Messi amepachika wavuni mabao 51 na kutoa pasi za usaidizi wa mabao 19 na amefunga mabao 12 Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu uliopita.
Kwa upande wa timu ya taifa Messi aliisaidia timu yake ya taifa ya Argentina kumaliza nafasi ya tatu katika michuano ya Copa America na kuondolewa kishingo upande na kuishia kuilaumu shirikisho la soka America Kusini CONMEBOL kuwa hawajawatendea haki.