PATRICE EVRA KAOMBA NAFASI YA KUINUSURU MAN UNITED
Wakati kocha wa zamani wa Manchester United Jose Mourinho akisema timu ya Manchester United hii ya sasa ni mbovu kuliko ya msimu uliyopita, beki wa zamani wa timu hiyo Patrice Evra ameomba apewe nafasi kusaidia.
Evra ,38, kupitia ukurasa wake wa twitter hajaweka wazi anatamani kurudi Man United kuisaidia katika nafasi gani zaidi ya kuandika ujumbe mfupi twitter katika ukurasa wake katika picha yake aliyokuwa amevalia jezi ya Man United na kubusu nembo (logo) ya timu hiyo.
.
“Nafikiri ni wakati wa kutoa uchafu mikononi mwetu, Bodi ya Man United mpo tayari kutuacha tuwasaidie?”
.
Kauli hiyo ya Evra inakuja msimu huu Manchester United ikiwa nafasi ya 8 katika Ligi Kuu England, ikicheza michezo sita, sare mbili na imepoteza miwili huku ikipata ushindi
katika michezo miwili huku ikicheza soka lisiloleta matumaini.
Evra amewahi kuchezea klabu ya Manchester United kwa miaka 8 (2006-2014) hadi anaondoka katika klabu hiyo alikuwa kacheza michezo 278 ya Ligi Kuu Uingereza kati ya hiyo akishinda 187, akipoteza 147 na amefunga mabao 7.
Kama Evra ataaminiwa na kupewa nafasi ya uongozi ndani ya Manchester United ataungana na Eric Abidal ambaye nae kaaminiwa na klabu yake ya zamani ya Barcelona na kupewa uongozi.
