FIFA kubadilisha magoli ya penati.
Shirikisho la soka Duniani FIFA wanampango wa kuondoa magoli yanayofungwa baada ya mchezaji kukosa penati.
Sheria hiyo itakuwa endapo mchezaji akapiga penati akakosa, hataruhusiwa kumalizia, ile timu iliyookoa itapewa ‘free kick ‘.
Hivyo sheria ingekuwa imeshapita, goli la hivi karibuni lililofungwa na Paul Pogba dhidi ya Everton baada ya kipa kuokoa penati yake lisingekuwepo.
Kingine ambacho kimeripotiwa kutaka kurekebishwa na watengenezaji wa sheria za mpira wa miguu (IFAB) ni kuondoa suala la kupoteza muda uwanjani, wakitaka kuondoa timu kufanya mabadiliko katika dakika za mwisho za mechi.
Wazo lingine lililoletwa ni wachezaji wanapofanyiwa mabadiliko, watoke uwanjani kupitia sehemu yoyote ambayo ni karibu na kutoka uwanjani na sio kutokea sehemu ya benchi la ufundi.
Kikao cha kujadili hayo kinataraji kufanyika hivi karibuni jijini London na watengenezaji wa sheria za mpira wa miguu (IFAB) ndipo watafanya uamuzi wa kuhusu kuyapeleka mapendekezo hayo katika kupigiwa kura mwezi Machi mwakani