WATFORD WAKUTANA NA KIPIGO CHA MWIZI TOKA KWA CITY
Septemba 14 2019 klabu ya Manchester City katika mchezo wake wa Ligi Kuu nchini England ilijikuta ikipoteza kwa mabao 3-2 dhidi ya Norwich, kitu ambacho kiliwaumiza sana wachezaji wa mabingwa hao watetezi.
Baada ya kipigo hicho kiungo wa Manchester City Rodri alisema wataenda kumuua mpinzani wao ajaye kwani kocha wake Pep Guardiola aliwaambiwa hii timu hairuhusiwi kufungwa.

“Kiukweli,unapopata michezo unapoteza basi mchezo ujao unamuua mpinzani, hivyo tunaenda kuperform katika mechi, tutawaua wapinzani wetu, Pep ametuambia hii timu hairuhusiwi kufungwa, tunatakiwa tushinde” alisema Rodri

Kwa kauli hiyo unaelewa tu Man City hawakufurahishiwa na kitendo kufungwa kwa rekodi ya kukaa mechi 9 bila kufungwa ndio maana jana Watford amekutana na kigipio cha goli 8-0 , Bernaldo Silva akipiga Hat-trick, na magoli mengine yakifungwa na Sergio Aguero, Otamendi, David Silva na Riyad Mahrez.