UONGOZI WA FA, PL NA EFL WAFANYA KIKAO NA TWITTER KUJADILI KUBAGULIWA KWA WACHEZAJI
Mamlaka za soka nchini England, (chama cha soka FA, ligi kuu na EFL )zimekutana na kufanya kikao na viongozi wa mtandao wa kijamii wa twitter kwa ajili ya kujadili namna watavyoepuka ubaguzi wa rangi kwa wachezaji kupitia mitandao ya kijamii.
Hatua hiyo imefikiwa baada ya viongozi hao wa soka kuona baadhi ya wachezaji msimu huu wamekutana na changamoto hiyo ya ubaguzi wa rangi kwa mashabiki kupitia mtandao wa twitter.

Baadhi ya wachezaji waliokutana na changamoto hiyo ni Kurt Zouma na Tammy Abraham wa Chelsea, Paul Pogba na Marcus Rashford wa Man United.
Kikao hicho kilichofanyika jana Ijumaa jijini London, England twitter wamekiri kuwa wanalishughulikia huku mamlaka za soka zikishinikiza kutaka kuona sheria kali zikichukuliwa ili kukomesha vitendo hivyo.
Taarifa ya FA inasema “ Kikao kilikuwa kizuri na chenye mafanikio, na kimewapa mamlaka za soka na Twitter fursa kupima/kuchunguza tabia hii isiyokubalika mtandaoni na nje ya mtandao.”