Pogba anasema nafurahia ninachoelekezwa na Mourinho
Manchester United leo wapo Turin Italia kucheza mchezo wao wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Juventus huo ukiwa ni mchezo wa marudiano, kivutio cha mchezo huo pia atakuwa ni Paul Pogba ambaye atakuwa anarudi Turin kucheza dhidi ya Juventus akiwa na jezi ya Manchester United lakini aliwahi pia kuichezea Juventus.
Paul Pogba mara kadhaa amekuwa akihusishwa kuwa katika mpango wa kuihama Manchester United kutokana na kudaiwa kuwa katika mahusiano mabaya na kocha huyo, hivyo kurudi kwake Turin leo kunatazamiwa kunaweza kuwa na mapokezi chanya kutoka kwa mashabiki wa Juventus.
Kuelekea mchezo huo Pogba baada ya kuhojiwa amesisitiza kuwa mahusiano yake na kocha Jose Mourinho yapo vizuri licha ya watu kuendelea kuripotiwa tofauti “Mimi ni mchezaji nafanya anachonitaka nifanye , yeye ni boss (Mourinho) na ndio kocha namsikiliza na nafanya hivyo nikiwa na furaha kabisa” alisema Pogba.
Leo Manchester United watakuwa katika uwanja Juventus Turin Italia kucheza mchezo wa round ya nne wa Kundi H linaloongozwa na Juventus walioshinda michezo yote mitatu ya mwanzo kwa kuwa na alama 9, wakifuatiwa na Manchester United wenye alama nne baada ya kushinda mchezo mmoja, sare mchezo mmoja na wamepoteza mchezo mmoja Old Trafford dhidi ya Juventus October 23 2018 kwa goli 1-0, huku Valencia wakiwa nafasi ya tatu kwa alama 2 na Young Boys wakishika mkia kwa kuwa na alama moja.