MAX TAYLOR KASHINDA MAPAMBANO YA KANSA NA KURUDI MAN UNITED
Kansa ni miongoni magonjwa hatari sana kwa binadamu na yamekuwa yakigharimu maisha ya watu wengi.
Beki wa Manchester United wa kikosi cha chini ya umri wa miaka 23 Max Taylor ,19, amefanikiwa kupambana na ugonjwa huo na kushinda.
Taylor aliwasili Man United 2014 na 2018 ndio alisaini mkataba wake wa professional lakini mwezi Februari mwaka huu alilazimika kusimama kucheza soka na kuanza matibabu ya kansa.
Kwa sasa Max Tayrol ameanza mazoezi mapema wiki hii baada ya matibabu yake ya kansa yaliomgharimu karibia miezi 9.