IRAN YAFUNGIWA SHIRIKI MCHEZO WA JUDO BAADA YA KUMSHINIKIZA MCHEZAJI KUPOTEZA MECHI
Kukiwa na katazo la mwanamichezo yeyote wa Iran kutoshindana na dhidi ya wale kutoka Israel, aliyekuwa bingwa ntetezi wa mchezo wa judo Saeid Mollaei alipoteza mchezo wake wa nusu fainali dhidi ya Khasan Khalmurzaev ili kukwepa kutana na Muisraeli Sagi Muki likiwa ni shinikizo toka nchini kwake.
Saeid amekuwa akiishi nchi Ujerumani kuanzi apoteze mchezo huo na alisema hamufurahi kupoteza pambano hilo kwani alikuwa amejiandaa kutetea ubingwa wake na medali yake ya pili ya dhahabu ila alihofia usalama wa familia yake.
Kamati kuu ya Olympic na Shirikisho la Kimataifa la Judo mapema mwaka huu ziliikemea vikali Iran na shirikisho la judo kwemda mbali zaidi kuifungia kwa madai ya nchi hiyo kutoonyesha nia ya kuacha vitendo hivyo.