RICCIARDO: BADO NIPO SANA RENAULT
Dereva wa timu ya Renault amesema kamwe hajutii uamuzi wake wa kuondoka RedBull na kujiunga na timu hiyo kwani alifanya uamuzi huo kwa kudhamiria na sio kwenda kukaa katika timu kwa muda na kuondoka bali kufanya jambo kwa mafanikio na malengo.
Dereva huyo Muaustralia bingwa mbio mara 7 alijiunga timu hiyo kwa mkataba wa miaka miwili 2019 – 2020 mkataba wenye dhamani ya zaidi ya dola millioni 50.
Timu ya Renault iliyomaliza katika nafasi ya 4 maimu uliopita wa mwaka 2018, ilianza msimu huu kwa lengo la kuwa katika timu 3 bora ila hadi sasa zikiwa zimebakia mbio 7 wanashika nafasi ya 5 nyuma ya Mercedes, Ferrari, RedBull na MacLaren ambao ni wateja wa injini zao. Swala hili halionyeshi kumkatisha tamaa Ricciardo ambaye anaamini ataendelea kuwepo katika timu hii wakiendelea kuonesha juhudi.