Ni kwa nini Barcelona imeshafuzu kuingia hatua ya 16 Bora klabu bingwa Ulaya msimu huu.
Kwa sasa Barcelona wana pointi 10. Endapo watapoteza mechi zao zote mbili zilizobaki watakuwa na pointi hizo hizo 10, halafu Inter akashinda mechi zake zote mbili zilizobaki inamaanisha atakuwa ana pointi 13, na hivyo Spurs ambaye sasa ana pointi 4 hataweza kufikisha pointi 10 alizonazo Barca kwa maana tayari ameshafungwa na Inter. Hivyo Barca watakuwa wapili , Inter wa kwanza.
Endapo Spurs atashinda mechi ijayo dhidi ya Inter Wembley, atakuwa na Pointi 7 sawa na Inter, Halafu Barca afungwe na PSV , kundi litakuwa linaonesha Barca wana pointi 10, Inter 7,Spurs 7.
Mechi za mwisho Spurs akaenda kushinda dhidi ya Barca Camp Nou, Inter akamfunga PSV , kundi litaonesha kuwa Inter wana pointi 10, Spurs 10, Barca 10.
Katika klabu bingwa Ulaya mkilingana pointi kitu cha kwanza wanachotizama ni mlivyokutana matokeo yalikuwaje (Head to Head ), Inter na Barca kwa hapo wakiwa wamelingana Pointi 10 kwa 10, watatizama timu hizi zilivyokutana matokeo yalikuwaje, ambapo matokeo yanaonesha walivyokutana katika mechi mbili Barcelona ameshinda kwa Aggregate ya 3-1, mechi ya kwanza Barca walishinda 2-0, ya pili jana wakatoka sare ya 1-1, hivyo Inter Milan atakuwa ameaga mashindano.
Hivyo basi, Barcelona hata akipoteza mechi zote 2 alizobakisha, amekwishafuzu hatua ya 16 Bora.