PEP GUARDIOLA ANAIANZA CHAMPIONS LEAGUE AKIWA NA MSONGO WA MAWAZO
Kocha Mkuu wa Manchester City Pep Guardiola anaanza mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya ugenini dhidi ya Shaktar Donetsk huku akiwa na mtihani katika safu yake ya ulinzi.
Guardiola ana wakati mgumu baada ya kikosi chake kukumbwa na lundo la majeruhi na sasa imethibitika kuwa beki wake John Stones atakuwa nje ya uwanja kwa muda wa mwezi mmoja akiuguza maumivu ya misuli.
Taarifa hizo zinakuja ikiwa ni siku kadhaa zimepita toka ithibitike kuwa mchezaji wao Aymeric Laporte anatazamiwa atakuwa nje ya uwanja miezi 6 akiuguza jeraha la goti, kwa upande wa John Stones aliyeumia mazoezini Guardiola amethibitisha kuwa atakuwa nje ya uwanja mwezi au wiki tano