ALEX MORGAN ASEMA HAMUOGOPI CRISTIANO RONALDO
Mshindi wa kombe la Dunia Mmarekani Alex Morgan ameweka wazi kuwa hahofii kukutana na nyota wa Juventus Cristiano Ronaldo katika tuzo za FIFA Septemba 23, Milan licha ya kumkosoa staa huyo wa Ureno siku za nyuma.
Kupitia akaunti yake ya twitter, Alex Morgan aliweka makala maalum yenye kichwa cha habari ‘Ronaldo ni Icon wa rushwa katika michezo’.
Makala hii aliiweka siku chache baada ya taarifa kutoka kuwa Ronaldo hatakabiliwa na kesi ya ubakaji aliokuwa ametuhumiwa kuufanya mwaka 2009 kufuatia kukosekana na ushahidi wa kutosha.
Ronaldo na Morgan watakutana uso kwa uso mjini Milani Septemba 23 katika tuzo za FIFA ambapo Ronaldo anawania tuzo ya mchezaji bora wa kiume huku Morgan akiwania tuzo ya mchezaji bora wa kike.
“Sitazamii kukabiriana nae tofauti” Morgan aliiambia Sports Illustrated.
“ Sifikirii kwamba mara nyingi katika hali ya sasa wanawake wanapaza sauti, na ni muhimu kuwasaidia. Na ninafikiri watu wengi kwa sasa wanajiuliza nani yupo sahihi na nani hayupo sahihi.
“Unapoangalia stori ya Ronaldo, ninafikiri kuna ushahidi mwingi wa kuthibitisha, na ninafikiri mwisho wa siku pesa imesaidia kuizima stori hii” amesema Morgan.
Morgan anasema kuwa mashitaka ya Ronaldo yalitupwa ili aendelee kucheza mpira ukizangitia ni mchezaji maarufu zaidi duniani.
Mmarekani huyo anasema alistushwa kusoma makala nyingi zikionesha kuamini kuhusu kilichoamuliwa juu ya shitaka hilo na ndipo akaamua kusema kupitia twitter na kupata maneno mengi mabaya kutoka kwa mashabiki wa Ronaldo.
Morgan mwishoni amesisitiza kuwa, ukosoaji wake kwa Ronaldo haufanyi aone Mreno huyo si moja ya wanasoka bora duniani.