Humud Abdulahim kujibu mapigo ya KMC
Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii leo aliyekuwa mchezaji wa KMC Humud Abdulahim, ambaye jana ilitoka taarifa rasmi kupitia msemaji wa klabu ya KMC iliyopanda daraja msimu huu Walter Harrison kuelezea sababu za kwanini Humud aliandika barua rasmi ya kuomba kuvunja mkataba wake na klabu hiyo, ameandika taarifa za kujibu tuhuma hizo na kuahidi kutolea ufafanuzi siku ya kesho kwa vyombo vya habari
“Nimesikia kilichozungumzwa na Team ya KMC ambayo nilikuwa mchezaji wao kabla sijavunja mkataba nao, ni zaidi ya mwezi mmoja sasa kuna vingi vimesemwa ambavyo sio vyakweli. Na kuna vingi havijasemwa ambavyo ni vya kweli Mungu akipenda kesho siku ya Alhamis majira ya saa Tano kamili Asubuhi nitazungumza na waandishi wa habari wa Media zote TV, Radio na Magazeti kuelezea sababu za mimi kuvunja mkataba na KMC nakutolea ufafanizuzi wa hicho walichoamua kunichafua mimi kwani swala hilo limelenga kunishushia heshama yangu katika jamii, familia na setka ya mpira wa miguu.kwa maslahi binafsi ya wachache ndani ya Team hiyo ya KMC ningependa na naomba wandidishi wahabari wote kufika…….“ameandika Humud Abdulahim