BIANCA AFUTA NDOTO ZA SERENA WILLIAMS US OPEN 2019
Mwanadada Bianca Andreescu anaandika historia yake na kupeperusha ndoto za Serena Williams.
Bianca ,19,ameibuka bingwa wa michuano ya US Open 2019 baada ya kumfunga Serena Williams kwa seti 6-3,7-5 katika mchezo wa fainali. Bianca anachukua ubingwa huo ikiwa ni mara yake ya kwanza kucheza fainali ya Grand Slam
Bianca anakua Mcanada wa kwanza kushinda ubingwa wa Single wa Grand Slam huku Serena kwa mara nyingine akishindwa kuifikia rekodi ya Margaret Court ya kushinda Grand Slam 24.
Hii ni mara ya pili mfululizo Serena Williams,37,anapoteza fainali ya US Open, mwaka jana alifungwa na Mjapan Naomi Osaka.